Meal Cellulose Tablet
Viungo:
Water Soluble na Insoluble meal cellulose
Kazi Na Faida Zake
- Kuweka sawa msukumo wa chakula tumboni na kutunza afya ya tumbo
- Kupunguza viwango vya cholesterol mwilini
- Kusaidia kupunguza viwango vya sukari katika damu
- Inasaidia kupunguza uzito.
Yafaa Kutumika Kwa:
- Watu waliofunga choo, kuharisha sugu, maumivu ya tumbo na ugonjwa wa "diverticular disease"
- Watu wenye kiwango kikubwa cha lipids
- Watu wenye kiwango kikubwa cha sukari au type 2 diabetes
- Watu wenye uzito mkubwa au wenye nia ya kupunguza uzito.
Maelezo Muhimu:
Meal Cellulose au Dietary Fiber:
Meal cellulose, au dietary fiber inajumuisha sehemu zote za mimea inayoliwa ambazo haziwezi kumeng'enywa au kufyonzwa na mwili. Kwa hiyo inapita ikiwa nzima tumboni, kwenye utumbo mdogo, utumbo mkubwa na nje ya mwili. Kwa jinsi hii, inaweza kufikiriwa kuwa haina faida yo yote, lakini ni ya muhimu sana katika kuziweka afya zetu vizuri.
Soluble Fiber au Insoluble Fiber:
Fiber kwa kawaida hugawanywa kwenye makundi mawili, ile inayoyeyuka kwenye maji (soluble fiber) na ile ambayo haiyeyuki kwenye maji (insoluble fiber).
Soluble fiber inayeyuka kwenye maji na kutengeneza kitu mfano wa jeli. Inaweza kusaidia kupunguza cholesterol na sukari katika damu. Soluble fiber inapatikana katika shayiri, njegele, maharagwe, tufaha (apples), matunda ya jamii ya machungwa, na karoti.
Insoluble fiber husaidia kutiririka kwa chakula ndani ya mfumo wa mmeng'enyo wa chakula na kuongeza kiasi cha kinyesi, kwa hiyo ni ya manufaa kwa watu wenye tatizo la kukosa choo au kutopata haja kubwa ya kawaida. Ngano nzima, mbegu na mboga nyingi ni vyanzo vizuri vya insoluble fiber.
Kuboresha Mtiririko Wa Chakula Na Kutunza Afya Ya Viungo Vya Kutiririsha Chakula
Meal cellulose inaongeza uzito na ukubwa wa kinyesi na kukilainisha. Kinyesi kikiwa kwa wingi ni rahisi kupita, na kupunguza uwezekano wa tatizo la kukosa choo. Kama tumboni kuna kinyesi kidogo na laini, meal cellulose itasaidia kukikausha kwa sababu inafyonza maji na kuongeza uwingi wa kinyesi. Inaweza kupunguza uwezekano wa kupata hemorrhoids (bawasili) na vifuko vidogo kwenye utumbo mpana (diverticular diseases).
Inazimua carcinogen, Inapunguza uzito wa carcinogen na kupunguza muda wa sumu kukaa ndani ya utumbo, inasaidia kupunguza kutokea kwa kansa ya utumbo mpana na kansa ya mkundu.
Kupunguza Cholesterol Katika Damu:
Soluble fiber katika Meal Cellulose inasaidia kupunguza viwango vya cholesterol katika damu kwa kupunguza lipoprotein nyepesi, au viwango vya cholesterol mbaya "bad cholesterol". Utafiti umeonyesha kuwa kuongezeka kwa fiber katika chakula kunaweza kupunguza pressure, ambayo inasaidia kulinda afya ya moyo.
Kusaidia Kupungza Sukari Katika Damu:
Soluble fiber inaweza kupunguza ufyonzwaji wa sukari, jambo ambalo kwa watu wenye kisukari linaweza kuwapunguzia sukari katika damu. Chakula chenye insoluble fiber kimehusishwa na kupungua kwa kujitokeza kwa type 2 diabetes.
Kusaidia Kupunguza Uzito:
Meal cellulose inaleta hali ya kujisikia umeshiba na chakula chenye uwingi wa fiber kina nishati kwa kiwango kidogo, kwa maana kwamba kina kalori kidogo kwa ukubwa ule ule wa chakula. Kutumia meal cellulose kabla ya kupata chakula kunasaidia kuweka uzito wa mwili kwenye kiwango kizuri.
<<<<< MWANZO